Malinzi aipongeza Yanga

Image caption Rais wa TFF,Jamal Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Yusuf Manji kufuatia timu yake kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.

Katika salamu zake za pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo muhimu na sasa wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya kimataifa barani Afrika mwakani.

Klabu ya Young Africans imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu nchini kwa mara ya 25 (ishirini na tano) mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Polisi Morogoro katika uwanja wa Taifa huku ikiwa na michezo miwili mikononi kabla ya ligi kumalizika.

Timu ya Azam, ikiwa na pointi 45 na michezo mitatu mkononi na Simba (ikiwa na pointi 41 na michezo miwili mkononi) zinagombania nafasi ya pili na ya tatu