Yanga kutawazwa mabingwa Mei 6

Image caption waziri Fenela Mukangara wa kwanza kushoto akiikagua timu ya Real Madrid (wastaafu) walipokuja Tanzania kucheza mechi ya kirafiki

Waziri wa Habari, Vijana Utamuduni na Michezo nchini Tanzania , Dr. Fennela Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania hapo Mei 6, 2015 baada ya kuisha kwa mchezo kati ya mabingwa wapya, Yanga na waliokuwa mabingwa watetezi, Azam FC.

Mechi hiyo haitakuwa na athari yoyote kwa Yanga kwa kutia doa sherehe za ubingwa wao hata kama Azam itashinda, kwani tayari wana pointi 55,ambazo hakuna timu yoyote inayoweza kuzifikia.

Makabidhiano ya kombe hilo yatafanyika katika uwanja wa taifa wa Dar es Salaam mbele ya mashabiki wapatao 50,000.

Tayari sherehe hizo zimeanza katika matawi mbalimbali ya timu hiyo, ambayo mwakano itashiriki kombe la Washindi barani Afrika.