Steve Bruce: Pointi zaidi zinahitajika

Haki miliki ya picha 1
Image caption Klabu ya Hull City

Meneja wa Timu ya Hull city amesema timu yake inahitaji alama zaidi katika michezo yake minne iliyobaki ili kujihakikishia nafasi ya kubaki katika ligi.

Hull City waliofanikiwa kuwachabanga Liverpool kwa bao 1-0 siku ya jumanne na kujikusanyia jumla ya 34 na kushika nafasi ya 15 nyuma ya timu mbili zitakazo shuka daraja.

"bado tunakazi ya kufanya nadhani pointi 34 hazitoshi kwa upande wetu”.

Wiki hii kuna baadhi ya wachezaji watakatwa ,mishahara yao kwa asilimia 40-50 kama tutaenda chini.

Hull wakiwa katika nafasi ya 15 wanapishina kwa alama nane tu na timu inayoburuza mkia ya Burnley wenye alama 26