Liverpool yachapwa na Hull City 1 - 0

Haki miliki ya picha z
Image caption Wachezaji wa Liverpool wakipewa maagizo na kocha wao

Liverpool imezidi kujiweka katika hali ngumu ya kuingia katika nne bora ya ligi hiyo baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila kutoka kwa Hull City.

Kipigo hicho cha ugenini walichokipata vijana hao wa Anfield kinawafanya waendelee kubaki nafasi ya tano na pointi zao 58 nyuma Manchester Utd yenye pointi 65.

Ligi hiyo itaendelea tena leo hii kwa mchezo mmoja kupigwa wakati Chelsea itakapokuwa ugenini kukipiga dhidi ya Leicester City.