Pacquiao atamba kumchakaza Mayweather

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mpambano kati ya Mayweather na pacquiao unasubiriwa kwa hamu duniani kote

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya dunia kushuhudia mpambano wa karne wa mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao,Bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao ametamba kumchakaza mpinzani wake kwenye mpambano utakaofanyika Mei 2 mwaka huu katika ukumbi wa Mgm Grand Vegas

Akiwa amezungukwa na mamia ya washabiki wake Pacquiao aliwaeleza "msiwe na wasiwasi mimi ndie ninae pigana na nina uhakika asilimia mia moja wa kushinda".

"Naamini huu ndio muda wa Mayweather kupoteza mchezo kwa mara ya kwanza’’

Floyd Mayweather hajawahi poteza mchezo katika mapambano 47 aliyokwisha cheza ,Huku Pacquiao akiwa kapoteza mapambano 5 na kutoka sare mara 2 katika mapambano 64 aliyocheza.