Southampton yalenga Ligi ya Mabingwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uwanja wa nyumbani wa Southampton

Klabu ya Southampton ina malengo ya kushiriki michuano ya klabu bigwa ndani ya miaka mitano kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji Les Reed.

Southampton au Saints wako nafasi ya saba katika msimamo wa ligi ya England wakiwa wamevunja historia yao kwa kujikusanyia alama nyingi zaidi msimu huu.

Reed ameeleza: "Tunafikiri tuna muundo mzuri wa kushiriki michuano ya ligi ya mabigwa wa ulaya ndani ya miaka mitano, Lakini ni muhimu kwetu kujiweka katika timu sita bora katika kipindi hicho ."

Wakiwa chini ya meneja Ronald Koeman wamekua na msimu mzuri na kama wakifanikiwa kumaliza katika nafasi sita za juu watashiriki michuano ya Europa ligi msimu ujao.

Mkurugenzi huyu akaongeza kwa kusema" kama itakua ni kitu kibaya kwetu kama tutashindwa kushiriki michuano ya ulaya kwa msimu huu.

Mafanikio ya timu hii yamekuja huku wakiwa wamewauza wachezaji wao muhimu wa kikosi cha kwanza mwanzoni mwa msimu Luke Shaw, aliyekwenda Man United Adam Lallana,Rickie Lambert na Dejan Lovren waliosajiliwa na Liverpool huku Calum Chambers akisajiliwa na Arsenal.