Novak Djokovic ajitoa michuano ya Madrid

Haki miliki ya picha Getty
Image caption nyota wa tenesi Novak Djokovic

Nyota wa mchezo wa tenesi Novak Djokovic amejiondoa kushiriki michuano ya wazi ya madrid .

Djokovic amejitoa ili aweze kujiandaa na michuano ya wazi ya Ufaransa na ile ya Rome Masters, itakayofanyika mwishoni mwa mwezi mei.

Taarifa iliyotolewa kwa waandaaji inasema kuwa “atakua na mapumziko ya muda kabla ya kuendelea na ratiba ya kalenda yake ya michezo”.

Mchezaji huyu bigwa wa michuano ya wazi ya Australian amekua katika kiwango bora msimu huu na kuwa mchezaji wa kwanza kushinda mataji matatu ya Master kwa msimu mmoja.