Roach :Mayweather hakutaka hili pambano

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Manny Pacquiao na Floyd Mayweather watapambana wikiendi hii

Kocha wa bondia Manny Pacquiao ,Freddie Roach ana wasiwasi huenda bondia Floyd Mayweather asitokeea kwenye mpambano wa mei 2.

Roach amesema “Sidhani kama mabondia wana hofu ila sidhani kama Mayweather alitaka kupigana alilazimishwa kupigana pambano hili na hakulitaka.

"Sijui kwanini amekua mkimya sana kwenye mpambano huu maneno yake yana woga”

Hata hivyo Mayweather hakushangazwa na kauli hizo za kocha huyo na kudai "nitakuepo niliongea uchafu siku za nyuma lakini hili pambano linajiuza lenyewe”.

Pambano hili limeteka hisia kwa washabiki wa masubwi duniani kote huku homa ya mchezo ikiwa inapanda kila muda unavyozidi kukaribia pambano hilo hapo Mei 2.