Nigel Pearson aomba radhi

Image caption Kocha wa Leicester City Nigel Pearson

Meneja wa Leicester City Nigel Pearson ameomba radhi kwa mwandishi wa habari aliyemtukana.

Pearson ameomba radhi kwa Ian Baker aliyemtolea maneno machafu baada ya kumuliza swali kuhusu madhaifu ya wachezaji wake yaliyosababisha timu kuboronga msimu mzima.

"Namuomba msamaha Ian ,Nilitaka kufanya hivyo mara moja mbele ya camera sikua na furaha kwa sababu ya kupoteza mchezo"alieleza kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

Na kwa upande wake Ian Baker amekubali kupokea msamaha huo baada kocha huyo kufanya hivyo.