Manny Paqcuiao na Mayweather kupigana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ukumbi wa pigano

Pigano ambalo limesubiriwa kwa miaka linatarajiwa kuanza katika mji wa Las vegas nchini marekani muda mfupi unaokuja,

Takriban watu 17,000 watafurika katika ukumbi wa MGM mjini humo kutizama pigano kati ya bondia Mmarekani Floyd Mayweather na Mfilipino Manny Pacquiao.

Watu wengi mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria pigano hilo.

Tiketi za pigani hilo zinauzwa tena kwa maelfu ya dola huku mamilioni ya watu wakitarajiwa kutizama moja kwa moja pigano hilo