V Persie anyimwa haki za kupiga Penalti

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Louis Van Gaal

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amempokonya mshambuliaji wa kilabu hiyo Robin Van Persie haki za kupiga mkwaju wa penalti baada ya kukosa mkwaju kama huo katika mechi dhidi West Brom.

Alipoulizwa iwapo Van Persie angeendelea kama mchezaji aliyeorodheshwa kupiga penalti kwa niaba ya kilabu hiyo alijibu ''hapana,amefika mwisho wake.Kila mara anarejelea makosa hayo hayo aliongezea''.

''Wayne Rooney pia amekosa mkwaju wa penalti na unapokosa mkwaju huo basi ujue utapiga foleni''.,aliongezea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Van Persie

Ushindi wa West Brom ulikuwa matokeo mabaya kwa upande wa Manachester United kwa mara ya tatu mfululizo.

Van Persie mwenye umri wa miaka 31 alikuwa na fursa ya kusawazisha kufuatia bao la Chris Brunty kunako dakika ya 63 baada ya refa Anthony Taylor kumpata na Saido Berahino na makosa ya kuunawa mpira katika eneo la hatari.