Yanga ilijituma licha ya kufungwa

Image caption Kikosi cha watoto wa Jangwani Yanga

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm amesema licha ya kufungwa na Etoile du Sahel nchini Tunisia na kutolewa katika michuano ya Shirikisho barani Afrika, wachezaji wake wamejituma uwanjani.

Yanga imerejea leo Dar es Salaam kutoka Tunisia baada ya kufungwa 1-0 katika mechi ya marudiano ya hatua 16 bora.Kutolewa kwa Yanga kunatokana na matokeo ya 1-1 ya mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.

Pluijm amesema Yanga imecheza mchezo mzuri sana ila mchezo haukuwa upande wao.Yanga, baada ya kutolewa, mwakani itashiriki michuano ya kombe la washindi barani Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara.