Cosafa itaijenga Stars kwa CHAN, AFCON

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kocha wa Taifa Stars Mart Nooij

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij amesema michuano kombe la COSAFA itakayofanyika nchini Afrika Kusini Mei 17 itaisaidia timu yake katika kujiandaa na Michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) na kombe la Mataifa Huru ya Afrika (Afcon).

Taifa Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya COSAFA, ambapo nchi nane zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali, nchi nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles, Swaziland.

Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.

Haki miliki ya picha bbc

Nooij amesema kuwa michuano hiyo itakuwa ni kama sehemu ya maandalizi.

Michuano ya CHAN itafanyika mwaka 2016 na Stars ipo kundi moja na Uganda wakati ile ya Afcon itafanyika mwaka 2017

Kombe la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.