Timu ya Kenya ya Raga yawasili UK

Image caption Timu ya mchezo wa raga ya kenya

Timu ya Kenya ya raga ya wachezaji saba maarufu Shujaa, imewasili jijini Glasgow nchini Uingereza huku ikijiandaa kwa michuano ya HSBC world sevens series itakayochezwa katika miji ya Glascow na London wikendi hii.

Mkufunzi Felix Ochieng amefanya mabadiliko kwenye kikosi chake kinachoshikilia nafasi ya kumi na tatu kwenye jedwali hilo kufuatia msururu wa matokeo duni.

Miongoni mwa wachezaji waliosafiri na timu hiyo ni nahodha Collins Injera, Humphrey Kayange Daniel Sikuta - Mwamba Dennis Ombachi Michael Wanjala - Pan Africa Strathmore Leos Tony Opondo - Billy Odhiambo - Oscar Ayodi - Bush Mwale - Augustine Lugonzo na Biko Adema -

Kenya itajibwaga uwanjani siku ya jumamosi kuchuana na New Zealand, Afrika kusini na baadaye kufunga kazi dhidi ya Samoa.