Rwanda kuwakumbuka wanamichezo

Rwanda inategemewa kuandaa michuano ya mpira wa mikono kwa ajili ya kuwakumbuka wadau wa mchezo huo waliokufa katika mauaji ya kimbari nchini humo.

Habari kutoka Rwanda zinasema timu kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi Ethiopia na Jamhuri ya watu wa Congo zimealikwa.

Hata hivyo, katibu mkuu wa chama cha mpira wa mikono cha Tanzania (TAHA), Nicholus Mihayo amesema hawajapata mualiko rasmi wa kushiriki.

“Tungependa kuwa sehemu ya mashindano hayo muhimu lakini mpaka sasa hatuna taarifa rasmi”, alisema Mihayo.

Habari kutoka ‘The Rwandan Focus’ zinasema maandalizi nchi hizo zimealikwa na itakuwa ni heshima kuwakumbuka wahanga.