Uganda mwenyeji riadha Afrika

Image caption Wanariadha wakikimbia mbio za nyika.

Uganda itakuwa mwenyeji wa michuano ya riadha ya Afrika (Pan Africa championship) itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu huku nchi kadhaa za Afrika, ikiwemo Tanzania zikitazamiwa kushiriki.

Michuano hiyo itafanyika katika jiji la Kampala Mei 31 huku wakimbiaji wakishiriki katika mbio fupi na ndefu.

Shirikisho la riadha Tanzania (AT), kupitia katibu mkuu wake, Suleiman Nyambui limesema litapeleka wakimbiaji katika mbio hizo mashuhuri.

Miongoni mwa wakimbiaji wa Tanzania wanaotegemewa kushiriki ni pamoja na Fabian Joseph, Mary Naali, Natalia Elisante na Ismail Juma.

Nchi nyingi, ikiwemo Kenya zinategemewa kushiriki kwa sababu michuano hiyo itakuwa ni sehemu ya kufuzu kucheza Michezo ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika Congo Brazzaville kuanzania Septemba 4-19 mwaka huu