Noij kutaja kikosi cha Stars

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Mart Nooij kocha wa Taifa Stars

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij Alhamisi anategemewa kutangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kuanza mazoezi kujiandaa na kombe la COSAFA litakayofanyika nchini Afrika Kusini Mei 17.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto amesema kuwa Nooij atakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za TFF kwa ajili ya kutangaza timu na mikakati yake kuelekea michuano hiyo.

Stars imepanda kundi B lenye timu za Lesotho, Madagascar na Swaziland. Stars itacheza na Swaziland Mei 18, na baadaye kucheza na Madagascar Mei 20 na kufuatiwa na mechi ya Lesotho Mei 20.

Nchi shiriki ni pamoja na Marutius, Namibia, Seychelles.

Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.