Tanzania yaelemewa gofu ya vijana Afrika

Image caption Mcheza gofu akiwa mazoezini

Tanzania imeshindwa kushiriki michuano ya gofu ya Afrika ya vijana inayofanyika Lusaka, Zambia kutokana na wachezaji wake kuwa shuleni

Makamu wa Raisi wa Chama cha gofu nchini Tanzania (TGU), Joseph Tango amesema wachezaji waliowategemea kushiriki wamebanwa na masomo mashuleni.

“Hii michuano inayohusisha timu za vijana na vijana wetu, wanaocheza katika vilabu vya TPC na Lugalo wamebanwa na masomo wakijiandaa na mitihani”, amesema Tango.Michuano hiyo imeanza siku chache zilizopita na itaisha Ijumaa.

Afrika Kusini, ikiwa na rekodi ya kushinda michuano hiyo mara 16, ni miongoni mwa timu shiriki ikiwemo Uganda, iliyomaliza nafasi ya 5 katika michuano iliyopita.

Zimbabwe, Zambia, Reunion, Kenya, Tunisia, Swaziland, Namibia, Botswana, Mauritius na Malawi ni miongoni mwa timu zinazoshiriki michuano hiyo mara kwa mara.