Ni vita ya Barcelona na Bayern Munich

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Timu ya Bayern Munich

Kocha Pep Guardiola anarejea Nou Camp kuiongoza Bayern Munich dhidi ya timu yake ya zamani Barcelona kwenye Nusu Fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa ni mwaka 2013, katika mchezo wa Nusu Fainali ya Mashindano haya, Bayern Munich, waliwachapa Barcelona Jumla ya Bao 7-0 katika Mechi mbili.

Barcelona wameifunga Bayern Munich mara 1 tu katika Mechi 8 zilizopita za Ulaya na kutoka sare 2 na kufungwa 5.

Mechi hii inakutanisha makocha,waliokuwa wachezaji wa zamani wa Barcelona Luis Enrique wa Barcelona na Pep Guardiola kwa upande Bayern Munich.

Mchezo huu utachezwa kwenye dimba la Nou Camp, huko Hispania.