Man United yamsajili Memphis Depay

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Memphis Depay akiwa amezifumania nyavu

Manchester United imefikia makubaliano kumsajili mshambuliaji Memphis Depay toka PSV Eindhoven ya Uholanzi.

Ada uhamisho wake inasemekana kuwa kati ya pauni milioni 25 hadi 30 na atasaini mkataba hadi mwaka 2019 huku kukiwa na nyongeza ya mwaka mmoja zaidi.

Depay anatarajiwa kupimwa afya yake wiki ijayo na atajiunga rasmi na man united mwezi juni dirisha la uhamisho likifunguliwa rasmi.

msimu huu, depay ameifungia psv bao 21 na kuisaidia kutwaa ubingwa wa holland.

Akithibirisha kuhama kwa Depay, mkurugenzi wa michezo wa psv Marcel Brands akiongea kwenye tovuti ya klabu hiyo na kusema wamempa baraka mchezaji huyo kuhama.

Depay ameichezea Psv jumla ya michezo 104 na kufunga mabao 42.