Man United,Burnley na Stoke zashinda

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Van Gaal

Marouane Fellaini alifunga bao la ushindi katika kipindi cha pili cha mechi dhidi ya Crystal Palace na kuipatia Manchester United ushindi wa kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Ashley Young ndiye aliyesaidia pakubwa katika mabao yote mawili baada ya kumnawisha mpira beki wa Crystal Palace na kupata penalti iliofungwa na Juan Mata na baadaye kutoa pasi nzuri iliotiwa kimywani na Fellaini kunako dakika ya 77.

katika matokeo mengine

Everton 0 - 2 Sunderland

Aston Villa 1 - 0 West Ham

Hull 0 - 1 Burnley

Leicester 2 - 0 Southampton

Newcastle 1 - 1 West Brom

Stoke 3 - 0 Tottenham