Afrika Kusini bingwa wa kuogelea

Image caption Muogeleaji akiogelea kwa mtindo wa kipepeo

Michuano ya kuogelea ya Kanda ya 4 Afrika imemalizika mjini Luanda, Angola huku Afrika ya Kusini ikiibuka kidedea. Nchi nyingine zilizoshiriki ni Mauritius, Msumbiji, Botswana, Uganda, Kenya, Tanzania na wenyeji Angola

Zaidi ya washiriki 2,00o walishindana katika aina mbalimbali (categories) za mashindano hayo kama vile michezo ya butterfly mita 200, free style ya mita 100 na mita 200 kwa mchezaji mmoja mmoja (individual).

Habari kutoka Luanda zinasema katika matokeo ya ujumla kwa upande wa wanaume, Afrika ya Kusini imeongoza, ikifuatiwa na Angola, Kenya, Botswana, Zambia, Msumbiji, Uganda, Mauritius na Tanzania ikiwa ya mwisho

Kwa upande wa wanawake, Afrika ya Kusini iliongoza, ikifuatiwa na Zambia, Angola,Mauritius,Kenya, Msumbiji,Botswana, Tanzania na Uganda

Katibu Mkuu wa chama cha kuogelea nchini Tanzania (TSA), Noel Kiunsi alikuwa na mategemeo ya timu yake kufanya vizuri lakini mambo yamekwenda tofauti.