Simba kuwaacha wachezaji kutoka Uganda?

Image caption Danny Sserunkuma (kulia), mmoja wa wachezaji wa Uganda.

Timu ya Simba ya Dar es Salaam huenda ikaachana na wachezaji wageni kutoka Uganda iwapo tu mawazo ya kocha mkuu wa klabu hiyo kutoka Serbia, Goran Kopunovic yatatekelezwa na uongozi wa timu hiyo.

Kocha huyo amesema haoni kama wachezaji hao wanafaa kuichezea Simba ila asingependa kuongea zaidi maada hata yeye mkataba wake umekwisha, hajui kama atabaki au la.

Habari zinasema kutoks vyombo vya habari zinasema kuwa Simba wameachana na mfungaji bora wa zamani wa Ligi Kuu ya Kenya, Danny Sserunkuma baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Habari zinasema kuwa mshambuliaji huyo raia wa Uganda aliandika katika ukurasa wake wa twitter akisema kuwa amefikia maamuzi ya kusitisha mkataba na hata ichezea Simba katika msimu ujao.Sserunkuma alisajiliwa na Simba mwezi Desemba mwaka jana akipewa mkataba wa miezi 12 ambayo ilikuwa inatarajiwa kumalizika mwaka huu.

Hadi anaondoka Simba SC, Sserunkuma aliyetokea Gor Mahia ya Kenya alikuwa amecheza mechi 17 na kuifungia mabao matano katika mashindano yote ikiwemo ligi kuu iliyomalizika hivi karibuni huku Yanga ikitwaa ubingwa.

Habari kutoka klabu ya Simba, ambayo imemaliza nafasi ya tatu katika ligi iliyoisha ni kwamba kocha mkuu, Goran Kopunovic amesema anahitaji kubaki na wachezaji wawili tu wa kigeni katika kikosi cha msimu uliopita na kwa tafsiri hiyo, wachezaji wengine, Simon Sserunkuma na Joseph Owino, wote Waganda, nao huenda wakaondoka muda wowote.

Wachezaji wengine wa kigeni kikosini Simba SC ni Waganda pia, Juuko Murushid na Emmanuel Okwi, ambao huenda wakasalia katika kikosi hiko kwa ajili ya msimu ujao.