Mahakama kunusuru soka Hispania

Image caption Wanasoka wa nchini Hispania

Mahakama moja nchi Hispania imepiga marufuku mgomo uliokuwa unaandaliwa na muungano wa wana soka nchini humo ambao ulikuwa umepangwa kutekelezwa mwishoni mwa wiki hii.

Mgomo huo ulianza kuhamasishwa wiki iliyopita kufuatia hatua ya serikali ya nchi hiyo kutoa tamko la kurejea upya haki ya urushaji matangazo ya mpira.

Maamuzi ya mahakama hiyo yanatoa nafasi kwa pande zote mbili kuweka taratibu za namna ya kuutatua mzozo huo,ambao unatishia kuuzika mpira nchini humo na hata kuweka shaka ya kutooneshwa kwa mtanange baina ya timu mbili za Atletico Madrid na Barcelona.

Muungano huo wa wachezaji nchini Hispania, umesema kwamba serikali yao imejipanga kuweka mipango ya kisheria juu ya nini cha kufanya na kipi kisifanyike kuhakikisha kila klabu inalipa ushuru kuanzia vilabu vikubwa mpaka vya hadhi ya chini.