Petr Cech ruksa kuondoka Chelsea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Golikipa wa Chelsea Petr Cech

Golikipa Petr Cech anaweza kumaliza miaka yake 11 ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kuruhusiwa kufanya mazungumzo na timu inayomtaka.

Wakala ya kipa huyo Viktor Kolar,amethibitisha kuruhusiwa kufanya mazunguzo na timu yoyote inayomuhitaji .

“Nina thibitisha tumeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu inayomuhitaji Cech japo anamkataba unaomalizika mwishoni mwa mwaka”alieeza wakala wa kipa huyo.

Wiki iliyopita Kocha wa Chelsea Jose Mourinho alisema anamuhitaji kipa huyo kuendelea kuitumika klabu hiyo.

Cech mwenye miaka 32 alijiunga na Chelsea mwaka 2004 na amecheza michezo 16 katika michuano yote msimu huu, akiwa chaguo la pili mbele ya kipa namba moja Thibaut Courtois.