Sharapova, Kvitova watinga robo fainali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Petra Kvitova na Maria Sharapova watinga robo fainali ya michuano ya wazi ya Italia

Nyota wa mchezo wa tenesi dunia Maria Sharapova ametinga hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya italia

Sharapova ametinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa seti 6-3 6-3 dhidi ya mpinzani wake Bojana Jovanovski

Petra Kvitova raia wa Jamuhuri ya Czech nae ametinga kwenye robo fainali baada ya kupata ushindi wa seti6-3 6-2 kwa kumfunga Jelena Jankovic.

Simona Halep wa Romania alimshinda Venus Williams kwa seti 6-2 6-1, huku katika mchezo uliochukua muda wa saa tatu Carla Suarez Navarro, alimgaragaza vibaya mpinzani wake Eugenie Bouchard kwa jumla ya seti 6-7 (2-7) 7-5 7-6 (9-7).

Mchezaji namba moja Serena Williams alijiondoa kwenye mashindano baada ya kuumia kiwiko muda mfupi kabla kumkabili Christina McHale.