Man City yaichabanga Swansea 4-2

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Yaya Toure mshambuliaji wa Man City

Matokeo ya Mechi mbili za ligi kuu ya England zilizochezwa hapo jana,Manchester City iliwachabanga Swansea mabao 4-2 . Ni Wilfried Bony ambaye mnamo dakika ya 90 lililopigilia msumali wa moto kwa Swansea baada ya kufunga bao la nne.Lakini Yaya Toure yeye alizifumania nyavu mara mbili dakika 21 na 74. , James Milner naye akifunga mnamo dakika ya 36. Huku katika mechi ya pili Arsenal wakitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Man united,ambapo kwa matokeo hayo sasa Arsenal wanaendelea kujiimarisha katika nafasi ya tatu. Leo West Brom watakipiga na Chelsea katika dimba la The Hawthons.