Ramsey sasa ndio mkufunzi mkuu wa QPR

Image caption Chris Ramsey

Kilabu ya QPR imemuajiri Chris Ramsey kama mkufunzi mkuu kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Ramsey mwenye umri wa miaka 53 alipewa kazi hiyo hadi mwisho wa mwezi Februari baada ya Harry Redknapp kujiuzulu lakini alishindwa kuizuia kilabu hiyo kusalia katika ligi kuu ya Uingereza.

''Chris alipochukua ukufunzi wa timu hii tayari tulikuwa katika matatizo makubwa'', alisema mwenyekiti wa kilabu hiyo Tony Fernandes.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption wachezaji wa klabu ya QPR

Licha ya kushushwa daraja,sisi kama bodi tumefurahishwa na kazi ya Ramsey aliyofanya.

QPR imeshinda mechi tatu kati ya 14 zilizosimamiwa na Ramsey huku wakitarajiwa kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Leicester.