Sunderland wafurahia kuto shuka daraja

Image caption Kocha wa klabu ya Sunderland Dick Advocaat

Klabu ya Sunderland na Arsenal jana wametunushiana misuli baada ya kutoka 0-0 na hivyo kufanikiwa kuondoa mashaka ya kushuka daraja msimu huu katika ligi ya England.

Hata hivyo kwa matokeo hayo Arsenal wanashika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City katika ligi hiyo inayomalizika.

Hata hivyo katika mchezo huo Sunderland wanapaswa kujilaumu kwa nafasi ambayo walipata na kushindwa kuitumia kupitia mshambuliaji wake Steven Fletcher. Mlinda mlango Costel Pantilimon ndiye aliyeibuka shujaa katika mchezo huo kutokana na uwezo aliouonyesha kwa kuokoa hatari kadha ikiwemo mkwaju wa penati.