Mourinho na Hazard ndio bora EPL

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mourinho

Mkufunzi wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ametangazwa kuwa mkufunzi bora katika ligi ya Uingereza kwa mara ya tatu.

Akihudumia kipindi chake cha pili katika kilabu hiyo rais huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 52 aliiongoza Chelsea kubeba taji lao la kwanza la ligi ya Uingereza katika kipindi cha miaka mitano pamoja na kombe la Ligi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Eden Hazard

Kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard ambaye aliifungia Chelsea mabao 20 alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya Uingereza msimu huu.