Ferdinand azungumza kuhusu marehemu mkewe

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rio Ferdinand akiiechezea QPR

Aliyekuwa Nahodha wa timu ya soka ya Uingereza Rio Ferdinand amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kifo cha mkewe kilichosababishwa na saratani na kusema kuwa ulikuwa wakati mgumu katika maisha yake.

Akiandika katika gazeti la the sun, aliusifu ujasiri wa mkewe Rebecca Ellison ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 34 mapema mwezi huu.

Mlinzi huyo wa kiabu ya QPR pia alisema kwamba alihisi kufanya makosa wakati alipokosa baadhi ya mechi wakati timu yake ilipokuwa ikijaribu kuzuia kushushwa daraja.

Image caption Rio Ferdinand na marehemu mkewe

Mkewe ambaye alimuoa mwaka 2009 ,alifariki May mosi kutokana na saratani ya matiti.

Amewaacha watoto watatu ,Lorenz mwenye umri wa miaka tisa,Tate mwenye umri wa miaka sita na Tia mwenye umri wa miaka minne.