Ancelotti:Nikifutwa nitapumzika mwaka 1

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Carlo Ancelotti

Mkufunzi wa kilabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kuwa atachukua likizo ya mwaka mmoja iwapo atafutwa kazi na kilabu hiyo.

Ancelotti mwenye umri wa miaka 55 amesalia na kandarasi ya mwaka mmoja katika kilabu hiyo lakini hajui hatma yake.

Kocha huyo ataanzisha mazungumzo na Real Madrid wiki ijayo huku kukiwa na madai kwamba kocha wa Napoli Rafael Benitez anatarajiwa kumrithi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Carlo Ancelotti

''Tayari nimeamua kuhusu hatma yangu katika siku za usoni'',alisema Ancelotti.

''Nadhani tutatukana wiki ijayo ili kuweza kuweka wazi hatma ya klabu hiyo'',alisema Ancelotti ambaye amekuwa akihusishwa na kilabu ya Manchester City baada ya Real Madrid kuicharaza Getafe mabao 7-3.