Bolt ashinda mita 200

Image caption Mwanariadha raia wa Jamaica Usain Bolt ashinda mita 200

Mwanariadha raia wa Jamaica Usain Bolt ameshinda kwa urahis katika shindano lake la kwanza mwaka huu huko barani Ulaya japokuwa ameshindwa kuvunja rekodi yake ya sekunde 20, kwenye mbio za mita 200 za Golden Spike huko Ostrava Jamhuri ya Czech.

Katika shindano hilo lililofanyika jana Bolt alitumia sekunde 20.13 ikiwa ya rekodi yake ya dunia ya sekunde 19.19 akimbwaga mmarekani Isiah Young "huwezi ridhika kama sivunji sekunde 20" alisema Bolt ambaye anajiandaa kwa mashindano ya dunia yatakayofanyika Beijing mwezi August. Naye Asafa Powell ameshinda katika mbio za mita 100 akitumia sekunde 10.04.