Johnson Thompson apania kushinda

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashabiki wa riadha nchini China

Mwanadada raia wa Uingereza Katarina Johnson-Thompson, amesema atajisikia vibaya kama hata nyakua medali yake ya kwanza ya dunia.

Thompson anashiriki a mashindano yanayotaraji kufanyika Beijing China mwaka huu. Nyota ya Muingereza ilianza kung'aa zaidi mwezi March mwaka huu pale aliponyakua medali ya dhahabu katika mashindano ya ndani ya Ulaya.

Lakini kwa sasa anasema kiu yake ni kushinda mashindano hayo hali anayosema itakuwa imetimiza ndoto yake.