Afrika Kusini yakana kutoa hongo kwa FIFA

Image caption Afrika kusini

Afrika kusini imekana kwa mara nyengine tena kwamba ilitoa hongo ili kupewa maandalizi ya kombe la dunia la mwaka 2010.

Waziri wa michezo nchini humo Fikile Mbalula, amewaambia wanahabari kwamba Afrika kusini itashirikiana na wachunguzi kutoka Marekani lakini imekataa kuingizwa katikati ya ugomvi kati ya FIFA na Marekani.

Amesema kuwa dola millioni 10 zilizotolewa zilikuwa malipo ya kusaidia soka miongoni mwa raia wa Afrika wanaoishi katika visiwa vya Caribbean na yalilipwa miaka kadhaa baada ya michuano hiyo kuandaliwa na Afrika kusini.