Raheem Sterling kuelekea Old Trafford?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raheem Sterling

Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.

Hatahivyo Liverpool imesema kuwa haiko tayari kufanya biashara na wapinzani wao wakuu kutoka Kaskazini Magharibi.

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Luois Van Gaal anavutiwa na kasi ya mchezaji huyo na uwezo wake wa kuwaponyoka mabeki.

Sterling amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa kushinda mataji.