Liverpool kumsajili James Milner

Haki miliki ya picha PA
Image caption Milner

Liverpool imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza James Milner kutoka kwa kilabu ya Manchester City kwa uhamisho wa bure.

Liverpool tayari imekubali makubaliano ya kibinafsi na mchezaji huyo wa miaka 29 ambaye atajiunga na kilabu hiyo wakati kandarasi yake itakapokamilika katika uwanja wa Etihad tarehe mosi July baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu.

Milner ameshinda mataji mawili ya ligi ya Uingereza ,kombe la FA pamoja na kombe la ligi wakati wa miaka mitano aliyohudumu katika klabu ya Machester ity.

Haki miliki ya picha AP
Image caption James Milner

Ameichezea Uingereza mara 53 na kufunga mabao manane msimu uliopita.

Milner alijiunga na City kutoka Aston Villa mwaka 2010 baada ya kusajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 26 na aliyekuwa meneja Roberto Manchini.