Dimba la dunia la wanawake kuanza Canada

Haki miliki ya picha USA TODAY Sports
Image caption Dimba la dunia la wanawake

Michuano ya kombe la dunia la wanawake inatarajiwa kuanza baadaye hii leo nchini Canada, ikiwa ni michuano ya kwanza mikubwa ya kandanda kufanyika tangu shirikisho la soka FIFA kukumbwa na upepo mbaya wa kashfa ya rushwa.

Hii ndio michuano mikubwa zaidi kwa soka la wanawake duniani, zaidi ya watu bilioni moja wanatarajiwa kushuhudia michuano hiyo kwa njia ya televisheni.

Mechi ya ufunguzi itakuwa baina ya wenyeji Canada dhidi ya China.

Haki miliki ya picha Xinhua News Agency
Image caption Dimba la dunia la wanawake

Timu za Ujerumani, Marekani na Ufaransa zinapewa nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwenye michuano hiyo.

Waandalizi wa michuano hiyo wamekataa matatizo ya FIFA kuwachanganya kwenye shughuli za uaandaaji wa michuano hiyo.