Kocha wa Barcelona hajui hatma yake

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Enrique

Mkufunzi wa Barcelona Luis Enrique amekataa kujadili hatma yake ama kuthibitisha iwapo ataendelea kuifunza Barcelona licha ya kuipatia timu hiyo mataji matatu.Enrique,katika msimu wake wa kwanza kama kocha katika kilabu ya Barcelona baada ya kumrithi Gerardo Martino aliongeza kombe la vilabu bingwa baada ya kupata lile la Copa Del Rey pamoja na La liga kwa kuicharaza timu ya Juventus katika fainali iliochezwa katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.