Canada yaishinda China

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sinclair

Canada ambayo ndio mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia miongoni mwa wanawake walianza vizuri kwa kupata ushindi katika mechi ilioshabikiwa na wengi.

Zaidi ya watu elfu hamsini waliangalia mechi hiyo mjini Edmonton huku Nahodha wa Canada Christine Sinclair akifunga penalti dhidi ya China katika dakika za lala salama na kupata ushindi.

Uholanzi iliishinda New Zealand bao moja kwa sufuri katika mechi ya pili.

Ni michuano mikubwa ya soka ya wanawake huku takriban mataifa 24 yakishiriki.

Hadi watu bilioni moja wanatarajiwa kuangalia michuano hiyo katika runinga.