wanariadha wa Tanzania wajifua Eldoret

Image caption Wanariadha wa Tanzania, akiwemo Dickson Marwa (wa kwanza kushoto) wakiwa katika mashindano

Wanariadha nguli wa Tanzania wanategemewa kuweka kambi ya mazoezi Eldoret, nchini Kenya kwa ajili ya kujiandaa na michezi ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika nchini Congo Brazzaville mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Wanariadha hao ni Fabian Joseph, Fabiano Nelson na Bazil John. Kocha wa timu ya taifa iliyoweka kambi jijini Arusha, Kaskazini mwa Tanzania , Francis John amenukuliwa akisema kuwa kambia hiyo ya Kenya itawasaidia wachezaji hao kujiandaa vema na michezo hiyo ya Afrika itakayofanyika kuanzia Septemba4 mpaka 19.

Mbali ya wachezaji hao, wachezaji wengine, Dickson Marwa, Emmanuel Giniki na Catherine Lange wapo nchini China ikiwa ni sehemu ya maandalizi, kwa mujibu wa kocha huyo.

Michezo ya Afrika itashirikisha wana michezo zaidi ya 3,000 kutoka katika nchi za Afrika wakishindana katika michezo mbalimbali kama vile riadha, soka kwa wanawake na wanaume, mpira wa wavu, kuogelea na ngumi.