FIFA;mtuhumiwa ajisalimisha kwa polisi Italia

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Mfanyi biashara mmoja aliyekuwa miongoni mwa watu 14 waliotajwa katika kashfa ya rushwa amejisalimisha kwa polisi nchini Italia

Mfanyibiashara mmoja anayetuhumiwa kushiriki ufisadi na maafisa wa FIFA amejisalimisha kwa polisi nchini Italia

Mfanyibiashara huyo raia wa Argentina alitajwa na serikali ya Marekani miongoni mwa watu 14 kwa tuhuma za ulaji rushwa na ufisadi, alijipeleka mwenyewe kwenye kituo cha polisi Kaskazini mwa Italia.

Shughuli za kumhamisha hadi Marekani bwana Alejandro Burzaco zinatarajiwa kuanza wakati wowote kutokea sasa.

Kulingana na uchunguzi uliofanyika na shirika la upelelezi la Marekani FBI bwana Burzaco na maafisa wengine wawili wanadaiwa kutoa donge nono kwa maafisa wa FIFA ilikupewa haki miliki ya maonyesho ya mechi za kombe la dunia .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alejandro Burzaco anatarajiwa kuhamishwa hadi Marekani

Uchunguzi sambamba unaoendeshwa na idara za upelelezi za Argentina unaendelea.

Hata hivyo kampuni yake bwana Burzaco imekanusha tuhuma zote dhidi yake ikisema kuwa madai hayo si ya kweli.

Haifahamiki ni vipi bwana Burzaco alikwepa mtego wa polisi majuma mawili yaliyopita licha ya kuwa katika mkahawa uleule walikokamatwa maafisa 7 wa FIFA.