Fifa: Sepp Blatter kung’atuka Desemba

Image caption Rais wa Fifa Sepp Blatter ataachia ngazi tarehe 16

Raisi wa shirikisho la kandanda duniani Sepp Blatter ataachia ngazi ifikapo Desemba 16 ambapo mrithi wa kiti hicho atajulikana.

Blatter aliyetangaza kujiuzulu wadhifa wake ikiwa ni siku nne tangu kuchaguliwa tena kuliongoza shirikisho hilo kwa muhula watano.

Wanachama wote 209 wa Fifa wataalikwa Uswisi kwa ajili ya uchaguzi wa Rais mpya wa shirikisho hilo la soka.

Maamuzi ya mwisho ya tarehe ipi utafanyika uchaguzi itajulikana mwezi Julai ambapo kamati kuu ya Fifa itakapokutana.