Ubelgiji Kumkosa Fellaini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nyota wa Ubelgiji Marouane Fellaini

Timu ya taifa ya Ubelgiji ina wasiwasi wa kumkosa nyota wake Marouane Fellaini katika mchezo wa kuzufu kwa michuano ya ulaya.

Ubelgiji watakua na mchezo dhidi ya Wales siku ya Ijumaa katika kusaka tiketi ya kucheza Euro 2016.

Fellaini anasumbuliwa na maumivu ya nyonga iliyomsabaisha kutojumuika na wenzake katika mazoezi.

kocha wa kikosi hicho Marc Wilmots ameeleza kuwa wanasubiri kauli ya daktari wa timu ili kujua ukubwa wa tatizo na kama wataweza mtumia mchezaji huyu katika mchezo huo.

Fellaini alifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-3 dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kalenda ya Fifa.