Camara awa kivutio Yanga

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Lansana Camara(asiye na jezi-wa pili kulia) akiwa mazoezini

Kiungo Lansana Camara kutoka Sierra Leone amesema anafurahia mazoezi katika klabu ya Yanga na ana imani mabingwa hao wa Tanzania Bara watamsajili kwa ajili ya msimu ujao.

Lansana, ambaye alikuwa akiitumia klabu ya Umea FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Sweden, alikutana na kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm na kufanya naye mazungumzo kuelekea ndoto yake ya kutua katika klabu hiyo.

“ Nina furahia mazoezi yangu na mashabiki wengi wanakuja kutuangalia, hii inatia moyo”, amesema Camara, amambaye anafanya mazoezi na timu hiyo kwa sasa.

Yanga imeanza mazoezi Jumatatu wiki hii katika viwanja vya kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.

Mashabiki wengi na makocha wa Yanga, Mdachi Hans Pluijm na msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa wanaonekana kuvutiwa na mchezaji huyo mwenye umbo la kuvutia kisoka na wana imani ataisaidia timu hiyo endapo ataonekana anafaa.