Tanzania,Kenya kushiriki gofu Namibia

Image caption Mcheza golf akiwajibika.

Michuano ya gofu ya Afrika (African golf Jacket) itakafanyika Windhoek, Namibia huku nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania na Kenya zikitarajiwa kushiriki.

Nchi nyingine ni pamoja na Botswana, Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Swaziland na wenyeji, Namibia, ambao watagharamia wageni wao

Makamu wa raisi wa chama cha gofu nchini Tanzania (TGU), Joseph Tango amesema mchezaji Abbas Adamu kutoka Arusha, Kaskazini mwa Tanzania atakuwa ni miongoni mwa washiriki, baada ya kushinda mara mbili michuano iliyopita na akiwa miongoni mwa wachezaji wa daraja la juu (Division A).

Wachezaji wengine wawili watachaguliwa kutoka division B na C na Tango atakuwa kiongozi wa msafara. “Tuna mategemeo wachezaji wetu watafanya vizuri na kurudi nyumbani na ushindi”, amesema Tango.