Wilshere:Mimi ni Arsenal sitaki Man City

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Kiungo cha kati wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere amekariri ari yake ya kusalia Emirati licha ya Manchester City kummezea mate

Kiungo cha kati wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Jack Wilshere amekariri ari yake ya kusalia Emirati licha ya dukuduku kuwa wapinzani wao wakuu klabu ya Manchester City wanakamia kumsajili msimu ujao.

City waliomaliza katika nafasi ya pili msimu huu wako mbioni kuratibu mabadiliko ya vipengee vya kanuni ya shirikisho la soka nchini Uingereza itakayohitaji vilabu kuimarisha idadi ya wachezaji wa asili ya Uingereza.

Yamkini klabu hicho tajiri hakina budi ilakuwasajili wachezaji zaidi ya wawili baada ya kuondoka kwa James Milner na Frank Lampard.

"kwa hakika japo nimekuwa kisoka humuhumu nchini hamu yangu kubwa ni kusalia Arsenal katika msimu ujao''alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anayeichezea timu ya taifa ya Uingereza.

Wilshere alishiriki mechi 9 pekee msimu uliopita baada ya kujeruhiwa mguu na kulazimika kukaa nje kwa takriban miezi 6.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wilshere alishiriki mechi 9 pekee msimu uliopita

Kiungo huyo anasema ndoto yake kuu ni kuiga mfano wa mchezaji bora duniani Lionel Messi na

Andres Iniesta ambao baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu na kukosa makali walijifurukuta na kuibuka kuwa viungo dhabiti wa klabu bingwa barani Ulaya na Uhispania Barcelona.Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alinukuliwa akisema kuwa mchezaji huyo anahitaji takriban misimu miwili ilikupona kabisa jeraha lake linalomsumbua sana la kifundo cha mguu.