Ratiba ya mechi za EPL yatolewa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meneja wa Chelsea Jose Mourinho

Chelsea itaanza utetezi wa taji la ligi ya Uingereza wakati itakapoikaribisha nyumbani Swansea katika wikiendi ya tarehe 8-9 mwezi Agosti.

Manchester City iliomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal

Arsenal itaialika West Ham ,Liverpool ikienda Stoke,Newcastle itakabiliana na Southampton huku Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.

Bournemouth iliopandishwa daraja,Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa,Everton na Crystal Palace mtawalia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Manuel Pellegrini

Msimu huu utanza wiki moja mapema ikilinganishwa na msimu uliopita.