Kombe la Dunia Wanawake kuendelea

Image caption Wachezaji soka wanawake Ufaransa

England itakwaana na Norway katika mzunguko wa pili wa mpira wa wanawake wa kombe la dunia, baada ya kuichabanga mabao 2 kwa 1 timu ya Colombia na kumaliza mzunguko wa pili wa kundi F.

Timu ya England imepata kile wanachostahili baada ya mwanadada Carney kuifungia timu yake goli mnamo dakika ya 15 ya mchezo, na mwanadada Fara Williams akaongeza bao la pili kwa mpira wa penati , lakini Colombia hawakuonyesha udhaifu na kuweza kupata bao 1 la kufutia machozi kipindi cha majeruhi. Mwenendo wa mchezo wa mchezo kwa asilimia ni inaonyesha England walitawala mchezo kiujumla kwa asilimia 52% ndani ya dakika 90 za mchezo. Matokeo ya timu zingine zilizocheza hapo ni Australia, walitoka sare ya bao moja dhidi ya timu ya Sweden, Marekani waliwaaibisha wenyeji wao Nigeria kwa kuwafunga kwa bao 1-0, na Ufaransa wakaifunga Mexico mabao 5 kwa nunge.