Chelsea na Mancity zamwinda Alex Song

Haki miliki ya picha AP
Image caption Song

Chelsea na Manchester City zimefanya mazungumzo ya kumsajili Alex Song kutoka Barcelona kulingana na mtandao wa Sky Sports.

Vilabu hivyo viwili hususan vinamtaka Song kwa kuwa anafuzu kuwa mchezaji wa nyumbani licha ya kuichezea Cameroon.

Song ambaye ameichezea West Ham msimu uliopita kwa mkopo ana miaka miwili ya kandarasi yake na Barcelona.

Image caption song

Hatahivyo West Ham ina matumaini ya kumsajili mchezaji huyo,lakini duru za Sky zinaamini kwamba kuna vilabu kadhaa vilivyo na hamu ya kununua ikiwemo City na Chelsea.

Mchezaji huyo wa miaka 27 ambaye aliichezea klabu ya Arsenal kwa miaka sita kabla ya kuelekea Barcelona miaka mitatu iliopita alicheza mechi 28 za West Ham msimu uliopita.

Barcelona iliomnunua mchezaji huyo kwa pauni milioni 15 inaaminika kutaka kumuuza mchezaji huyo kwa pauni milioni 5.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Song

Kandarasi yake katika klabu hiyo ya Nou Camp inaaminika kuwa ya kitita cha pauni 70,000 kwa wiki.